Deus Kaseke na Yacouba Sogne leo wameungana na Michael Sarpong na Lamine Moro kuwa vinara wa mabao katika kikosi cha Yanga
Nyota hao wote wana mabao manne, Yacouba na Kaseke wakifunga leo katika mchezo dhidi ya Ihefu ambao Yanga iliondoka na ushindi wa mabao 3-0
Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda na Carlinhos wanafuata kwenye orodha ya wafungaji wakiwa wamefunga mabao mawili kila mmoja
Aidha kwa upande wa wapishi wa mabao, Yacouba anaongoza akiwa ametoa pasi nne za mabao akifuatiwa na Ntibazonkiza mwenye assisti 3 huku akiwa ndio kwanza ameichezea Yanga chini ya dakika 180
Tuisila Kisinda, Farid Mussa na Deus Kaseke pia wako katika orodha hiyo wakiwa nao wametoa pasi tatu za mabao kila mmoja
Yanga imefanikiwa kwa kucheza kitimu zaidi, takwimu za wafungaji pamoja na watoa pasi za mabao zinaashiria kuwa kocha Cedric Kaze amefanikiwa katika filosofia yake ya kutengeneza timu ya wachezaji 11 na sio timu ya watu 11