Mashabiki wa Yanga mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Sokoine hapo kesho kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kesho ni siku nyingine ya sherehe kwa Wanayanga pale uwanja wa Sokoine hivyo Wananchi wajae kwa wingi kuwapa sapoti mashujaa wao ambao wako ndani ya jiji la Mbeya tangu jana
Chama cha Sokoa mkoani Mbeya (MREFA) kimetaja viingilo vya mchezo huo ambapo wakubwa ni Tsh 8,000/- na Watoto ni Tsh 3,000/-
Katibu Mkuu wa MREFA Lucas Kubaja amesema wataanza kuuza tiketi kuanzia saa tano asubuhi
ADVERTISE HERE