Wakiwa wameshuka dimbani mara 16, Yanga wamekuwa na ufanisi zaidi wanapocheza ugenini kuliko wakiwa dimba la Benjamin Mkapa
Katika michezo minne ambayo Yanga wamepata sare, mechi tatu zilipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na mchezo mmoja kupigwa Mwanza
Yanga walilazimishwa sare katika michezo dhidi ya Tanzania Prisons, Simba na Namungo Fc zote jijini Dar es salaam wakati mchezo dhidi ya Gwambina Fc ulipigwa Misungwi, Mwanza
Ushindi wa michezo saba umepatikana ugenini au nje ya jiji la Dar es salaam wakati mechi nne wameshinda pale kwa Mkapa na mchezo mmoja kule Chamazi
Kesho Jumatano Yanga watashuka uwanja wa Sokoine kuikabili Ihefu Fc
Kwa takwimu hizi ni wazi Kocha wa Ihefu Fc Zuberi Katwila anafahamu ugumu wa kazi anayokwenda kukumbana nayo siku ya kesho
Kwani vijana wa Cedric Kaze hawana masihara kabisa katika mechi za huko mikoani