Msimu huu Yanga imebarikiwa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu maarufu kama mipira iliyokufa
Mwanzoni mwa msimu Wananchi walinufaika sana na uwepo wa Carlinhos ambaye ndie aliyekuwa bosi wa mipira hiyo
Ujio wa Saido Ntibazonkiza ni ongezeko la silaha nyingine katika eneo hilo
Tunaweza kusema huyu Ntibazonkiza ndio Mwalimu kabisa wa kupiga mipira hiyo
Wanayanga sasa hawawezi kuwa na presha ya kumkosa Carlinhos ambaye mpaka sasa hajafurahia maisha katika kikosi cha Yanga kutokana na kusumbuliwa na majeraha mara kwa mara

Carlinhos ameitumikia Yanga chini ya michezo mitano kutokana na changamoto hiyo
Kabla ya ujio wa Ntibazonkiza, ndiye aliyekuwa akitegemewa kupiga mipira yote ya adhabu
Katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji, Ntibazonkiza alifunga bao mahiri lakini pia akatengeneza bao jingine
Ujio wake ni faida nyingine kwa Yanga kwani sasa Wananchi wana uhakika wa kufunga mabao kupitia mashambulizi au mipira ya kutenga