Uongozi wa klabu ya Yanga umebaini uwepo wa jezi feki mikoa ya Mbeya, Rukwa, Shinyanga na mikoa mingine ya pembezoni mwa Tanzania
Taarifa iliyotolewa na Yanga mapema jana, mashabiki wameaswa kujiepusha na jezi hizo huku wakitakiwa kutoa taarifa ya wale wanaohusika na biashara hiyo ambayo inahujumu mapato ya klabu
Jezi halisi za Yanga zinapatikana nchi nzima zikiwa na vitobo vyenye umbo V pande mbili za ubavuni. Pia nembo ya Yanga na ile ya GSM zote ni za plastiki

Yanga imewaonya wauzaji na wasambazaji wa jezi hizo kuacha mara moja, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi watakapotiwa mikononi na vyombo vya Sheria
ADVERTISE HERE