Lamine Moro yuko kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu jana akiweka kambani bao lake la nne dhidi ya Dodoma Jiji
Tunaweza kusema huyu ni beki mshambuliaji kwani sasa anaongoza orodha ya wafungaji kwenye kikosi cha Yanga akifungana na Michael Sarpong ambaye pia ana mabao manne
Taratibu ameanza kumuambukiza pacha wake Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye nae jana kafungua akaunti yake ya mabao msimu huu
Lamine ni beki mwenye jicho la goli, huyu siku moja kocha Cedric Kaze ajaribu kumtumia kama mshambuliaji wa kati, anaweza kuwa hatari
Unaweza kumfananisha na nyota wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa marehemu Said Mwamba 'Kizota'
Kizota alikuwa sentahafu mahili lakini pia alikuwa ni mshambuliaji hatari
ADVERTISE HERE