Nani aanze, nani asubiri vs Dodoma Jiji leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2020
Nani aanze, nani asubiri vs Dodoma Jiji leo?

Wananchi wako Arusha, saa kumi jioni watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Yanga iko 'on-fire' kwani imeshinda mechi nne zilizopita huku ikiishushia Mwadui Fc kipigo cha mbwa koko katika mchezo uliopita, Wananchi wakishinda mabao 5-0

Kocha Cedric Kaze ameanza kufanikiwa kimbinu, sasa vijana wake hawamuangushi kwani ni mwendo wa kugawa dozi tu

Kikosi cha Kaze leo hakitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa. Ndivyo ilivyo, kocha hapaswi kubadili timu yake ya ushindi kama anataka kuendelea kupata matokeo

Mabadiliko pekee ambayo yanaweza kuonekana pengine ni kuanzishwa kwa Saido Ntibazonkiza ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Deus Kaseke katika kikosi kilichoanza mchezo uliopita

Pia, Kaze anaweza kumpa mapumziko winga Tuisila Kisinda ambaye alipata majeraha mchezo uliopita. Kisinda alirejea kikosini na alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshiriki mazoezi ya mwisho hapo jana. Kucheza kwake kutategemea na utimamu wake wa mwili

Ukuta wa Yanga unatarajiwa kuendelea kuwa salama chini ya Metacha, Kibwana, Yassin, Lamine na Mwamnyeto wakati pale kati mafundi Feisal Salum na Mukoko Tomombe wanaweza kuendelea kushirikiana

Farid Mussa alikuwa bora sana kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United, pengine leo anaweza kuwa na nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza

Yacouba ndio 'DJ wa Shoo' kwa sasa kwani uwepo wake pale mbele kwenye safu ya ushambuliaji umeipa Yanga mafanikio katika mechi nne zilizopita

Pamoja na kuwa mwenendo wake wa kuzifumania nyavu sio mzuri, Michael Sarpong ni mtu muhimu sana kwenye safu ya ushambuliaji

Sarpong ni msumbufu, mara nyingi amewaweka katika presha walinzi wa timu pinzani

Amekuwa na maelewano mazuri na Yacouba pamoja na Deus Kaseke aliyenufaika zaidi kupitia kwake kwani mara nyingi Kaseke huingia eneo la ushambuliaji pale Sarpong anapowahamisha mabeki pembeni

Leo ni mechi nyingine ambayo Wananchi wanasubiri kushangilia ushindi, hakuna shaka Kaze atashusha kikosi chake cha maangamizi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’