Hatutauza mchezaji wakati huu - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2020
Hatutauza mchezaji wakati huu - Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, ambaye pia ni Bosi wa Kamati ya Usajili Yanga Mhandisi Hersi Said amesema mpaka sasa mezani wana ofa za wachezaji watatu wanaotakiwa na timu nyingine

Hata hivyo Hersi amesisitiza kwa wakati huu hawako tayari kumuachia mchezaji wao yeyote wa kikosi cha kwanza kwani wanaweza kuvuruga malengo yao ya kujenga kikosi imara kwa ajili ya kuwania ubingwa msimu huu

Hivi karibuni ziliibuka tetesi kuwa klabu ya TP Mazembe imevutiwa na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' pamoja na beki kisiki Bakari Nondo Mwamnyeto huku Mcongomani Mukoko Tomombe akiivutia timu moja kutoka Arabuni

"Ni kweli wachezaji wetu wengi wanahitajika na timu nyingine, mpaka sasa tuna ofa kwa wachezaji watatu lakini huu sio muda sahihi wa kuwaachia wachezaji wanaoanza katika kikosi cha kwanza tupo katika kipindi cha kuijenga timu," alisema Hersi

GSM ndio wanaosimamia usajili wa Yanga, kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuimarisha kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria wakiwa vinara wa mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Kazi hawajamaliza GSM kwani wakati huu wa usajili wa dirisha dogo wanatarajiwa kushusha mashine nyingine za kazi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’