Omary Rashid (Chibada) anakuwa mchezaji wa kwanza wa Yanga B kunufaika na ujio wa kocha Cedric Kaze kwenye kikosi cha Yanga akipandishwa timu ya wakubwa
Habari njema kwa wachezaji wa timu ya vijana ni kuwa wanachopaswa kufanya ni kupambana, kujituma na kumuonyesha Mrundi huyo uwezo wao wa kulisakata gozi la n'gombe
Kaze amefundisha soka la vijana kwa muda mrefu, ni kocha anayependa kutengeneza wachezaji wake yeye mwenyewe
Baada ya kutua Yanga tu, Kaze alitembelea mazoezi ya timu ya vijana na baada ya siku chache akapendekeza wachezaji watano wapandishwe kwenye kikosi chake ili aweze kuwaangalia
Chibada ndiye aliyen'gara zaidi, hakumpandisha timu ya wakubwa kwa upendeleo
Amepewa nafasi kwenye mechi kadhaa za kirafiki, 'dogo' yuko vizuri, ni mchezaji anayeweza kuja kufanya vizuri sana huko mbeleni
Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema watampa nafasi mara kwa mara ili kuhakikisha wanamuimarisha zaidi