Mechi za mzunguuko wa 16 ligi kuu ya Vodacom zitaanza kuunguruma kesho Ijumaa kwa mechi nne kupigwa katika viwanja mbalimbali
Vinara wa igi hiyo Yanga shughuli yao itakuwa siku ya Jumamosi pale uwanja wa Sheikh Amri Abeid watakaposhuka dimbani kuikabili Dodoma Jiji
Yanga ndiye mwenyeji wa mchezo huu ambao uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria waliamua kuupeleka jijini Arusha kuwapa burudani wakazi wa jiji hilo na mikoa ya jirani
Yanga imepania kumaliza duru ya kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo, wamebakisha dakika 180 tu kukamilisha hilo
Mchezo wao wa mwisho kufunga duru hiyo utapigwa mkoani Mbeya dhidi ya Ihefu Fc

ADVERTISE HERE