Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina 'Chicken' amekutana na uongozi wa klabu ya Yanga kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya.
Lwandamina aliyetua jana Jumatatu kutoka kwao nchini Zambia alikokuwa mapumziko tangu kumalizika kwa msimu, amekutana na uongozi ili kuweka hadharani mikakati yake ya msimu wa 2017-18.
Pia mkutano huo umetumika na viongozi wa Yanga kuwasilisha majina ya wachezaji ambao klabu tayari imeshawasajili sambamba na kuangalia mustakabali wa baadhi ya wachezaji walipo kwenye kikosi cha kwanza na wale ambao majadiliano ya kuwasajili yanaendelea.
Yanga inatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu ya msimu mpya wakati wowote.
Kuhusu usajili, Katibu Mkuu Charles Mkwassa amesema zoezi hilo huenda likakamilika wiki ijayo ambapo baada ya kukamilika ndipo kikosi cha Yanga msimu wa 2017-18 kitawekwa hadharani.
Mkwassa amewataka mashabiki wa Yanga waendelee kuwa na utulivu kwani wako mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji watatu muhimu, mpaka wiki ijayo zoezi hilo litakuwa limekamilika.
Ili kuepuka kuvuruga mchakato, Mkwassa amegoma kutaja majina ya wachezaji hao hadi pale watakaposajiliwa rasmi.

ADVERTISE HERE