Baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United hapo jana, kikosi cha Yanga kinaelekea mkoani Arusha kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Disemba 19 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Yanga ni timu ya Wananchi, hivyo ni haki kwa Wananchi wa Arusha kupata burudani kutoka kwa timu yao
Mechi mbili zimesalia kukamilisha duru ya kwanza , Yanga ikicheza mechi 15 bila ya kufungwa
Hesabu za kocha Cedric Kaze ni kuhakikisha anamaliza duru ya kwanza bila ya timu yake kufungwa
Baada ya Dodoma Jiji, mchezo wa kukamilisha duru ya kwanza ni dhidi ya Ihefu Fc na utapigwa Disemba 26 mkoani Mbeya
ADVERTISE HERE