Zanzibar Heroes yairambisha urojo Bara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2017
Zanzibar Heroes yairambisha urojo Bara
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' iko hatarini kuondoshwa mapema kwenye michuano ya CECAFA Challenge baada ya leo kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa ndugu zao Zanzibar Heroes.

Kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza dhidi ya Libya, Kilimanjaro Stars ilikosa muunganiko kila mchezaji akicheza kivyake na kujikuta muda mwingi wakifukuza vivuli vya vijana wa Zanzibar Heroes waliokuwa moto.

Himid Mao alianza kuifungia Stars kwenye dakika ya 28 baada ya kupasiana vyema na Elias Maguri aliyemtengea pasi murua na akaukwamisha mpira wavuni kwa shuti kali.

Licha ya kutangulia kufungwa wachezaji wa Zanzibar Heroes iliyosheheni nyota wanaocheza ligi kuu ya Vodacom waliendelea kucheza kandanda safi na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Stars.

Baada ya kosakosa nyingi, Zanzibar Heroes ilijipatia mabao yake yote kwenye kipindi cha pili yakiwekwa kimiani na Kassim Khamis (70) na Ibrahim Ahmada (77)

Huo ni ushindi wa pili kwa Zanzibar Heroes baada ya juzi kuilaza Rwanda mabao 3-1.

Stars imebaki na alama yake moja iliyopata kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Libya.



Kikosi cha Zanzibar
Mohammed Abdulrahman, Ibrahim Mohammed Said, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Salum Kheri, Issa Haidar Dau, Abdulaziz Makame Hassan, Mohammed Issa 'Banka', Mudathir Yahya/Kassim Suleiman Khamis dk58/Ibrahim Abdallah Hamad dk87, Ibrahim Hamad, Feisal Salum Abdallah na Hamad Mshamata Makame.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’