Wananchi wanatamba kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 37 baada ya kushuka dimbani mara 15
Yanga imefunga mabao 22 huku ikiruhusu mabao matano tu, haijafungwa bao lolote katika mechi 10
Mshambuliaji Michael Sarpong ndiye anayeongoza kwa mabao akiwa amefunga mabao manne
Lamine Moro, Deus Kaseke na Yacouba Sogne wote wamefunga mabao matatu kila mmoja
Carlinhos, Mukoko Tomombe na Tuisila Kisinda wao wamefunga mabao mawili kila mmoja wakati Waziri Junior na Haruna Niyonzima 'Baba Mzazi' wao wamefunga bao moja kila mmoja
Kwa upande wa wapishi wa mabao, Yacouba Sogne yuko kileleni akitoa pasi nne za mabao
Tuisila Kisinda ana pasi tatu za mabao kama ilivyo kwa Farid Mussa mwenye assist tatu
Carlinhos ana assist mbili sawa na Deus Kaseke wakati Ditram Nchimbi, Kibwana Shomari na nahodha Lamine Moro wao wana assist moja kwa kila mmoja
Yanga ilianza msimu na kasi ndogo ya kufunga mabao lakini sasa ni wazi Wananchi wanatengeneza nafasi nyingi na hivyo idadi ya mabao wanayofunga itaendelea kuongezeka mechi hadi mechi