Injinia Hersi atambia kikosi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2020
Injinia Hersi atambia kikosi Yanga

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi wa Yanga kwa kazi kubwa wanayoifanya kuipambania timu

Hersi amesema furaha wanayopata Wananchi leo imetokana na jasho la vijana wa Cedric Kaze

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kaze ameandika;

"Pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi chini ya kocha Cedric Kaze na viongozi kwa ujumla wake kwa kutupambania wananchi"

"Raha hizi zinatokana na jasho la vijana hawa. Ama hakika tuna kikosi imara chenye talanta na uchu wa mafanikio walioamua kupambania nembo ya klabu yetu pendwa"

"Wananchi tumekuwa tukitamani sana mafanikio. Tumuombe mola atuongoze kwenye safari hii ya mafanikio na tuifike salama salmin. Kikubwa kama wanachama, mashabiki na wapenzi wa YANGA, tujitoe kuiunga mkono timu yetu na wadhamini walionyuma ya ujenzi wa timu yetu"

"Aidha, kuelekea Ujenzi wa kikosi imara chenye uwezo wa kutupa matokeo chanya hujengwa kwa umakini wakati wa usajili lakini pia uongozi mzuri wa Benchi na Miundombinu bora"

"Yote haya kwa pamoja huleta muunganiko wa kikosi imara bila kusahau MUDA WA MUUNGANIKO huo. Naweza kusema ni faraja kubwa kuanza kujenga kikosi imara na wakati huohuo kupata matokeo mazuri. Tusisahau wananchi tunajambo letu"

WE ARE ON TOP OF THE TABLE. ONTO THE NEXT ONE

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
58m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’