Daktari Yanga afunguka majeraha ya Kisinda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2020
Daktari Yanga afunguka majeraha ya Kisinda

Uongozi wa klabu ya Yanga umewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu hali ya winga Tuisila Kisinda ambaye alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Mwadui Fc hapo jana

Kisinda alifunga moja ya mabao matano ya Yanga katika ushindi dhidi ya Mwadui Fc, alishindwa kumaliza mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Farid Mussa

Daktari wa Yanga Dk Shecky Mngazija amesema nyota huyo alipata mshtuko wa goti na maumivu ya kawaida, wanaamini atakuwa sawa baada ya mapumziko ya siku chache aliyopewa

"Kisinda amefanyiwa uchunguzi wa kina, tumebaini alipata mshtuko wa goti baada ya kugongana na mchezaji mwenzake. Kwa sasa yuko sawa, maumivu aliyonayo yataisha kadri anavyoendelea kupumzika. Tunaamini ataweza kurejea mazoezi timu itakapokuwa mkoani Singida keshokutwa" alisema Dk Mngazija

Kisinda amejipambanua kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha Yanga, akiwa miongoni mwa wachezaji waliocheza dakika nyingi msimu huu

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’