Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze alifanya uamuzi sahihi wa kumteua Lamine Moro kuwa nahodha wa mabingwa hao wakihistoria akisaidiana na Bakari Nondo Mwamnyeto na Mukoko Tomombe
Lamine amekuwa kiongozi wa mfano awapo uwanjani. Pengine ndiye 'sentahafu' mwenye mabao mengi zaidi kwenye ligi kuu msimu huu
Jana katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc alifunga bao lake la tatu, lakini pia akatoa asisti kwa Yacouba Sogne aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0
Utulivu wa safu ya ulinzi ya Yanga unachangiwa na uwepo wa Mghana huyo akishirikiana vyema na wenzake pale nyuma
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Fergusson aliwahi kusema safu bora ya ushambuliaji itakupa uhakika wa kushinda mechi lakini safu bora ya ulinzi itakupa uhakika wa kushinda ubingwa
Mpaka sasa usemi huo umedhihiri kwani Yanga iko kileleni, mechi nyingi ilihitaji ushindi wa bao 1-0 tu kuondoka na alama zote tatu
Ni kutokana na uhodari wa akina Lamine, Metacha, Kibwana, Yassin, Mwamnyeto, Mukoko na nyota wengine ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye eneo la ulinzi
Katika mechi 10 kati ya 15 ambazo Yanga imecheza, haikuruhusu bao. Yanga imefungwa mabao matano tu msimu huu