Yanga imenoga sasa, taa ya kijani imewashwa kuelekea ubingwa wa 28 msimu huu!
Ushindi wa mabao 5-0 waliopata Wananchi hapo jana dhidi ya Mwadui Fc, umewafanya wajikite kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10 baada ya kufikisha alama 37
Wakati Wananchi wakitakata dimba la CCM Kambarage hapo jana, jukwaani alikuwepo mshambuliaji mpya wa timu hiyo fundi Saido Ntibazonkiza
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa katikati ya wiki inayoanza kesho, dirisha dogo la usajili litafunguliwa, Yanga ikitarajiwa kumuandikisha rasmi Ntibazonkiza
Ntibazonkiza alitua Yanga akiwa mchezaji huru hivyo baada ya kuandikishwa atakuwa na tuhusa ya kuwatumikia Wananchi
Vibali vya kazi vya nyota huyo viko tayari, hivyo bila shaka atawakabili Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi kuu unaofuata ambao utapigwa Disemba 19 kule mkoani Arusha
Ntibazonkiza hatakuwa mgeni kwenye kikosi cha Yanga kwani amejifua na Wananchi kwa takribani wiki mbili
Yanga hii ya Kaze, watu watateseka sana...!