Nani aanze, nani asubiri vs Mwadui Fc leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Dec 2020
Nani aanze, nani asubiri vs Mwadui Fc leo?

Leo ni nafasi nyingine kwa Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi wakihitaji ushindi dhidi ya Mwadui Fc huko mkoani Shinyanga

Kwa sasa ni kama kocha Cedric Kaze ameanza kupata kikosi chake cha kwanza, akishinda mechi tatu zilizopita bila ya kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi

Kaze anaweza kurejea na kikosi kilekile ambacho pia kilimpa ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting

Katika mchezo huo, Tuisila Kisinda na Deus Kaseke walitumika kama washambuliaji wanaotokea pembeni wakati Yacouba Sogne na Michael Sarpong wakisimama eneo la ushambuliaji wa kati

Safu ya ulinzi ya Yanga imekuwa bora tangu mwanzo mwa msimu, bila shaka Lamine, Mwamnyeto, Kibwana, Yassin na Metacha Mnata wataendelea kuunda ukuta wa chuma

Eneo la kiungo Feisal Salum na Mukoko Tomombe, nao wametengeneza pacha ya kipekee wakishirikiana karibu mechi zote msimu huu

Kwa hakika Wananchi hawapaswi kuwa na shaka juu ya kikosi chao kwani vijana wa Kaze wameiva na wako kamili kila idara

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’