Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amewataka wakazi wa mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kambarage kesho Jumamosi kuwapa sapoti wachezaji wao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc
Yanga iliwasili Shinyanga jana jioni na leo itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Kambarage
Mabingwa hao wa kihistoria wanaendelea na kampeni ya kukusanya alama tatu ili kuhakikisha mwishoni mwa msimu wananchi wanashangilia ubingwa wa 28
Mpaka sasa hesabu ziko salama kwani Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu



ADVERTISE HERE