Hatutawadharau Mwadui Fc - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2020
Hatutawadharau Mwadui Fc - Kaze

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema wachezaji wake wako tayari kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi, uwanja wa CCM Kambarage

Yanga iliwasili mkoani Shinyanga jana jioni na leo wanatarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo

Kaze amesema vijana wake wana ari kubwa ya kusaka alama tatu katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

"Kila mmoja anajua umuhimu wa mchezo wa kesho, sisi hatuangalii nafasi tuliyopo katika msimamo wa ligi, tunachohitaji ni alama tatu. Huu ni mchezo mgumu ugenini, tutapambana kusaka ushindi"

"Mwaka jana hata Simba walipoteza mchezo wao wa kwanza Shinyanga hivyo sisi hatuwezi kubweteka, tutapambana kuweza kupata alama tatu muhimu," alisema Kaze

Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi ya kipekee msimu huu, inaongoza ligi ikiwa na alama 34 lakini ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu

Kaze amepania kuweka rekodi ya kumaliza duru ya kwanza bila ya kufungwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’