Nyota mpya wa Yanga Saido Ntibazonkiza ni miongoni mwa wachezaji waliokwea pipa mapema leo kuelekea jijini Mwanza na wataunganisha safari mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amemjumuisha Ntibazonkiza katika kikosi chake cha wachezaji 24
Ntibazonkiza ataanza kuitumikia Yanga baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambapo anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Dodoma Jiji Disemba 19
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Jumatano ijayo Disemba 15, ambapo baada ya dirisha hilo kufunguliwa Ntibazonkiza ataruhusiwa kuwatumikia Wananchi
ADVERTISE HERE