Yanga leo inarejea mazoezini kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa Jumamosi, Disemba 12 uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze alitoa mapumziko ya siku mbili kwa wachezaji wake baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambao ulipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema leo vijana wanakamilisha maandalizi kabla ya safari ya mkoani Shinyanga ambapo wataondoka kesho Alhamisi kwa usafiri wa Ndege mpaka Mwanza kisha kuunganisha Shinyanga
Yanga itafunga mwaka nje ya jiji la Dar es salaam wakikabiliwa na mechi nne dhidi ya Mwadui Fc (Shinyanga), Dodoma Jiji (Arusha), Ihefu Fc (Mbeya) na Tanzania Prisons (Rukwa)
ADVERTISE HERE