Alianza msimu taratibu na kuwapa nafasi mabingwa wa ukosoaji kumshambulia kuwa hakustahili kusajiliwa na Wananchi
Alipotua kocha Cedric Kaze alitoa ufafanuzi kuwa mwamba huyu yuko vizuri, alipendekeza usajili wake kwa kuwa aliamini ataisaidia Yanga
Kilichomchelewesha kuonyesha ubora wake ni kukaa nje muda mrefu bila kucheza soka kutokana na changamoto ya corona iliyotikisha dunia mwanzoni mwa mwaka huu
Hapa tunamzungumzia mshambuliaji Yacouba Sogne aliyetua Yanga msimu huu akitokea klabu ya Asante Kotoko ya kule Ghana
Yacouba ni mmoja wa wachezaji walion'gara kwenye kikosi cha Yanga katika michezo mitatu iliyopita

Huyu mwamba ana kasi, nguvu na msumbufu sana anapokuwa na mpira
Ana uwezo mkubwa wa kukokota mpira na kuingia eneo la hatari la timu pinzani kwa kasi
Changamoto pekee inayomkabili ni kukosa umakini kwenye eneo la umaliziaji lakini kwa hakika sasa ameanza kuonyesha thamani yake
Kwa ujumla, kikosi cha Yanga kilianza msimu taratibu na sasa kimeanza kuimarika na kucheza kandanda linaloeleweka chini ya kocha Cedric Kaze
Kuna hatari huko mbeleni kuna timu zitatuzwa furushi la mabao pale safu ya ushambuliaji itakapokaa sawa