Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze aliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili
Taarifa iliyotolewa na Yanga imebainisha kuwa Kaze amewapa wachezaji ruhusu ya kwenda kuziona familia zao na watarejea mazoezini hapo kesho Jumatano kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya safari ya Shinyanga kupitia Mwanza siku ya Alhamisi
Disemba 12 Yanga itashuka uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kuumana na Mwadui Fc
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Arusha kwa ajili ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Yanga ikiwapelekea Burudani wakazi wa mkoa wa Arusha
Baadae vinara hao wa ligi wataunganisha mkoani Mbeya kuifuata Ihefu Fc
Disemba 31 Yanga itakamilisha mwaka 2020 kule Sumbawanga kwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons