Kiungo kiraka Deus Kaseke, chini ya kocha Cedric Kaze,amekuwa mchezaji muhimu sana katika kikosi cha Yanga
Ndani ya kikosi cha Kaze, Kaseke hana majukumu maalum, anazunguuka kila mahali
Anakaba, anashambulia na akipata nafasi anafunga. Huyu ndiye Kaseke aliyesajiliwa na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2015 akitokea klabu ya Mbeya City
Jana katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, kuna wakati alikaribia kutoka mchezoni hasa baada ya kukosa mkwaju wa penati
Sio vyema kumlaumu kwa kukosa penati kwani jambo hilo ni kawaida na limewatokea wachezaji wengi. Wanayanga waendelee kuthamini kazi kubwa anayoifanya uwanjani
Mechi mbili nyuma Kaseke ndiye aliyekuwa shujaa wa Yanga akifunga mabao mawili muhimu yaliyoihakikishia Yanga alama sita
Ni mchezaji ambaye ari yake iko juu sana. Ni aina ya wachezaji ambao wakati mwingine hawaonekani sana lakini kazi wanayofanya uwanjani ni kubwa