FT : Yanga 2-1 Ruvu Shooting

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2020
FT : Yanga 2-1 Ruvu Shooting

Ni mwendo wa kukusanya alama tatu tatu! Ndivyo unavyoweza kusema kwa mwenendo walionao Yanga baada ya kuichapa Ruvu Shooting mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Wale waliokuwa wakihoji uwezo wa Yanga ya Cedric Kaze bila shaka wameanza kupata majibu yao kwani kwa hakika Yanga imeanza kucheza vile ambavyo kila mmoja anapenda kuiona

Leo walinzi wa Ruvu Shooting wakongwe Juma Nyoso na Ponera wanaweza kulala na viatu kwani TK Master, Michael Sarpong na Yacouba Sogne waliwaweka katika wakati mgumu

Sarpong ndiye aliyetangulia kuifungia Yanga bao la kuongoza kwenye dakika ya 31 akimalizia mpira uliokuwa ukizagaa langoni kwa Ruvu Shooting

Bao hilo lilidumu mpaka wakati timu zinakwenda mapumziko

Baada ya ukosoaji mwingi kuwa Yanga 'inakata moto' katika kipindi cha pili, leo mambo yalikuwa tofauti kwani moto uliwawakia zaidi Ruvu Shooting kwenye kipindi cha pili

Presha ya Yanga walioiweka langoni kwa Ruvu Shooting mwanzoni mwa kipindi hicho, ilipelekea Wananchi kuzawadiwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Ruvu kuzuia kwa mkono shuti la Mukoko

Deus Kaseke alichukua jukumu la kupiga mkwaju huo lakini haikuwa bahati, hakufanikiwa kuuweka mpira kambani

Kwenye dakika ya 60, Ruvu wakarejea mchezoni kwa bao la Richard David aliyetumia makosa ya Mwamnyeto

Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Yanga ambayo ilikuwa ikilishambulia lango la Ruvu Shooting kama nyuki

Kama washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Sarpong, wangeongeza umakini, mabao yangekuwa mengi

Krosi ya Kisinda ambaye kwa hakika alikuwa nyota wa mchezo huo, iliwekwa kambani na mlinzi Ponera aliyejaribu kuokoa krosi hiyo matata huku akiwa katika presha kubwa kutoka kwa Sarpong

Ulikuwa mchezo ambao Yanga imedhihirisha sasa iko tayari kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Wananchi wameendelea kugoma kufungwa sasa wakicheza mechi 14 za ligi mfululizo bila kufungwa!

Wamejikita kileleni wakijikusanyia alama 34. Mechi tatu zimebaki kukamilisha duru ya kwanza. Mechi hizo ni dhidi ya Mwadui Fc, Dodoma Jiji na Ihefu Fc

Mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utapigwa Dar wakati michezo dhidi ya Mwadui na Ihefu inapigwa ugenini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’