Jioni ya leo Yanga itakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Ni mchezo ambao Wananchi watakuwa wakisaka alama nyingine tatu muhimu zitakazoendelea kuwaweka salama kileleni mwa msimamo wa ligi
Bila shaka, kiraka Deus Kaseke leo atakuwa na nafasi nyingine ya kuwapa furaha Wananchi
Katika michezo miwili iliyopita, Kaseke ndiye aliyewahakikishia Yanga alama sita akifunga bao katika kila mchezo dhidi ya Azam Fc na JKT Tanzania
Lakini pia, Kaseke ametengeneza ushirikiano mzuri na Yacouba Sogne na pengine wawili hao wanaweza kuanza pamoja kama ilivyokuwa katika michezo miwili iliyopita
Kocha Cedric Kaze anamtumia Kaseke kama mshambuliaji kivuli ambaye hushambulia mianya inayoachwa na walinzi wa kati wa timu pinzani