Kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama tayari amewasili Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi ya jeraha lililomuweka nje kwa takribani miezi sita
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema nyota huyo amewasili salama Afrika Kusini, atakuwa huko katika matibabu kwa muda wa wiki mbili
"Balama tayari ametua Afrika Kusini na leo (jana) ameanza matibabu yake ambapo tunatarajia atakuwa huko kwa muda wa wiki mbili au zaidi"
"Atarejea nchini Disemba 24, wapenzi na Wanachama wetu watapewa taarifa juu ya maendeleo yake," amesema Bumbuli
Aidha Bumbuli ametoa ufafanuzi kuwa Balama alipatiwa matibabu hapa nchini kama ilivyokuwa imependekezwa na madaktari lakini alipoanza mazoezi mepesi alikuwa akilalamika kusikia maumivu hivyo uongozi kuamua kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi