Uongozi wa klabu ya Yanga umepokea rasimu ya Mabadiliko kutoka kwa washauri wao Kampuni ya La Liga ambao wamekamilisha jukumu la kupendekeza mfumo bora wa uendeshaji
Hivi karibuni, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambao pia ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said alisafiri kuelekea nchini Hispania kwa ajili ya kukabidhiwa ripoti hiyo
Leo ameikabidhi kwa Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla katika Mkutano na Wanahabari uliofanyika Hoteli ya Serena
Akizungumza katika Mkutano huo, Dk Msolla amesema rasimu hiyo yenye kurasa 400 itaenda kuchakatwa katika Kamati ya Utendaji pamoja na Kamati ya Sheria na Kamati ya Mabadiliko kabla kupelekwa kwa Wanachama kupitia matawi nchi nzima ili utaratibu uwe shirikishi
Dk Msolla amesema mchakato huo utafuata sheria na taratibu zote za nchi kama ulivyoelelezwa na baadae wataitisha Mkutano Mkuu wa mwaka ili kupitisha Mabadiliko hayo
Dk. Msolla amemkabidhi rasimu hiyo Mshauri wa Yanga Senzo Mbatha ambaye watashirikiana nae kusimamia mchakato huo kuelekea Mkutano Mkuu wa Wanachama.
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, amesema Yanga inakwenda kuandika historia kwa kuwa klabu ya kwanza barani Afrika kuleta mfumo wa uendeshaji kutoka kwenye Dunia ya kwanza katika soka
"Leo Yanga tunaandika historia kwa kuleta mfumo wa uendeshaji wa klabu yetu kutoka kwenye Dunia ya kwanza kwenye soka kwa maana ya La Liga Hispania"
"Mfumo huu unakwenda kuirudisha klabu kwa wanachama na wao ndio watakuwa wamiliki halali wa klabu na baada ya mfumo kukamilika, niwahakikishie tu watu wote sio tu Tanzania bali Afrika nzima watakuja kwetu kujifunza," amesema Hersi
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko Wakili Msomi Alez Mgongolwa amesema vipaumbele vikubwa viwili viliyo katika rasmi hiyo ni mfumo imara wa uongozi na ushirishwaji wa Wanachama ambao watatambulika na mfumo
"Vipaumbele viwili kwenye rasimu yetu ya mfumo wa mabadiliko, kutakuwa na Menejimenti imara ili kuwa na taasisi bora lakini pia Wanachama wetu hatujawaacha nyuma, wao kitaalam wametambulika kama 'Fans Engagement' ambao wanatambulika rasmi na mfumo"