Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa mshambuliaji wake mpya Saido Ntibazonkiza atawasili nchini kesho Jumatano JNIA saa 3:20 usiku
Kama ilivyo kawaida ya Wananchi, Ntibazonkiza, anatarajiwa kupata mapokezi makubwa, wananchi wakiaswa kujitokeza kwa wingi
Ntibazonkiza anawasili mapema kuanza kujifua na kikosi cha Yanga ili awe tayari kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria pale tu dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa
Mchezo wake wa kwanza unaweza kuwa dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa Disemba 19 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Disemba 15 na habari njema ni kuwa wachezaji wanaosajiliwa katika kipindi hicho hawatasubiri tena mpaka dirisha lifungwe
Watakachohitaji ni barua ya uthibitisho wa usajili wao kutoka timu zao za zamani, jambo ambalo Ntibazonkiza halitamuhusu kwa kuwa alisajiliwa na Yanga akiwa mchezaji huru
Β