Siku ya Jumapili, Disemba 06, 2020 mabingwa wa kihistoria Yanga watakuwa na jambo lao pale uwanja wa Benjamin Mkapa watakapowakaribisha Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani kwani kikosi cha Ruvu Shooting msimu huu kimeimarika tangu walipomchukua Master Charles Mkwasa ambaye msimu uliopita aliitumikia Yanga akiwa kocha msaidizi
Wakati Yanga wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakikusanya alama 31, Ruvu Shooting wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 23 sawa na klabu ya Simba iliyofunga mabao mengi zaidi
Yanga imesalia na mechi nne kukamilisha duru ya kwanza, vijana wa kocha Cedric Kaze wakipania kumaliza duru hiyo wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kila mechi kwao ni kama fainali kwani kila wanaposhuka uwanjani, lengo kuu ni kuondoka na alama zote tatu
"Sisi tunachotaka msimu huu ni ubingwa, hivyo kwetu kila mchezo ni kama fainali. Tumejipanga kutimiza kiu yetu ya kutwaa ubingwa, " amesema
"Jumapili, tarehe 06/12 saa moja Kamili usiku Wananchi waje kwa wingi Uwanja wa Mkapa kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu dhidi ya Ruvu shooting"