Deus Kaseke ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Yanga kwa mwezi Novemba akichuana na Metacha Mnata, Bakari Nondo Mwamnyeto na Yacouba Sogne
Mwamnyeto ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho kwa mara ya tatu wakati mlinda lango Metacha Mnata anawania tuzo hiyo kwa mara ya pili
Sogne na Kaseke hii ni mara yao ya kwanza kuwania tuzo hiyo ambayo mwezi uliopita ilikwenda kwa Farid Mussa
Mpigie kura mchezaji unayedhani anastahili kushinda tuzo hiyo. Kura zinahesabiwa kupitia ukurasa wa Yanga mtandao wa Twitter yangasc1935
ADVERTISE HERE