Yanga sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili baada ya timu hiyo kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo uliopigwa Musoma, Mara
Timu zote zimeshuka dimbani mara 13, Yanga ikikusanya alama 31 wakati Azam Fc wana alama 26. Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 23
Jumamosi Yanga itakuwa na nafasi ya kuendelea kujiimarisha juu ya msimamo pale itakapoikabili Ruvu Shooting katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Taratibu Wananchi wanaanza kuyatengeneza mazingira ya ubingwa msimu huu
ADVERTISE HERE