Kwa sasa mashabiki wa Yanga wanafurahia maisha ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi. Baada ya kushinda mechi mbili zlizopita, Yanga imesimama pale juu ikiwa na alama 31, alama sita dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili
Azam Fc leo wanacheza na Biashara United mkoani Mara pasipo kuwa na kocha mkuu, Cioaba walimtimua baada ya kipigo cha Yanga
Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi zilizofanyikwa na kila upande kuanzia viongozi, wadhamini na mashabiki kuhakikisha Yanga inakuwa imara msimu
Yanga ndio timu pekee ambayo haijafungwa mchezo wowote msimu huu. Yani nyota wote wapya wa Yanga hawafahamu radha ya kufungwa ikoje
Tangu mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi, Yanga haijapoteza mchezo wowote iwe ligi au mechi za kirafiki. Wamecheza mechi zaidi ya 20 bila ya kufungwa. Ni bahati mbaya wachambuzi wa soka nchini huwezi kuwasikia wakizungumzia rekodi hii!
Silaha kubwa ya Yanga ni safu yake bora ya ulinzi, ambayo kwa hakika inakwenda kudhihirisha msemo wa kocha wa zamani wa Manchester United kuwa washambuliaji bora wanakupa uhakika wa kushinda mechi lakini walinzi bora wanakupa uhakika wa kushinda ubingwa
Mpaka sasa Yanga imeruhusu mabao manne tu baada ya kucheza mechi 13 kwenye ligi msimu huu
Msimu uliopita wakati kama huu Yanga ilikuwa tayari imefungwa mabao nane
Changamoto pekee ambayo hakuna shaka kocha Cedric Kaze ataipatia majibu ni idadi ya mabao machache ambayo Yanga inafunga
Kwa sasa mpango uliopo ni alama tatu, lakini hakuna shaka idadi ya mabao yanayofungwa itaongezeka, pengine safu ya ushambuliaji itaongezewa nguvu dirisha dogo