Beki wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amewatoa hofu Wananchi kuhusu afya yake baada ya kupata majeraha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, mchezo ambao Wananchi walishinda kwa bao 1-0
Kibwana amesema kuwa atarejea uwanjani hivi karibuni baada ya kutibiwa jeraha la bega alilopata kwenye mchezo huo
Kibwana aliyecheza mechi karibu zote za Yanga msimu huu, alikosa mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania kutokana na majeraha hayo nafasi yake ikichukuliwa na Paulo Godfrey 'Boxer'
Amesema kwa sasa anajisikia vizuri, matumaini yake ni kuwa atarejea uwanjani baada ya siku chache
"Kwa sasa ninaendelea vizuri na nina amini kwamba nitareja uwanjani hivi karibuni kuendelea na kazi ya kusaka ushindi kwa ajili ya timu yangu," amesema
Kibwana yuko katika msimu wake wa kwanza na kikosi cha Yanga akisajiliwa kutoka klabu ya Mtibwa Sugar
Amekuwa sehemu ya kikosi imara Yanga ambacho kimesimama kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 31