Kiraka Deus Kaseke ameshinda tuzo ya nyota wa mchezo dhidi ya JKT Tanzania baada ya kupigiwa kura kwa wingi na mashabiki wa Yanga
Kaseke amewashinda Yassin Mustafa na Tuisila Kisinda baada ya kupata kura asilimia 65 ya kura zote zilizopigwa
Kaseke ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania
Amekuwa na wiki nzuri kwani siku tatu nyuma aliingoza Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc, akifunga bao hilo
Hongera kwake Deda04, ni tuzo aliyostahili
ADVERTISE HERE