Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa JKT Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo Jumamosi
Deus Kaseka kwa mara nyingi ameipa Yanga ushindi muhimu baada ya kufunga bao pekee katika dakika ya 33 akimalizia pasi murua ya Yacouba Sogne
Kaseke na Yacouba anaonekana kuelewana vyema kwani hata bao alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc, pasi ya mwisho ilitolewa na Yacouba
Wachezaji wa Yanga leo watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi mnono kwani walitengeneza nafasi nyingi hasa katika kipindi cha kwanza




Ni ushindi muhimu kwa Yanga ambayo sasa imefikisha alama 31 na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Vijana wa kocha Cedric Kaze wameendeleza rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo mpaka sasa
Yanga sasa imecheza mechi 20 bila ya kufungwa ikiwa ni pamoja na michezo ya kirafiki