Kesho Yanga inaianza kampeni ya kusaka alama 15 kukamilisha duru ya kwanza ya mechi za ligi kuu ya Vodacom msimu huu kwa kuikaribisha JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Yanga ina nafasi kubwa ya kumaliza kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya duru ya kwanza kulingana na ratiba ya mechi zake zilizobaki ukilinganisha na wapinzani wao Azam Fc na Simba
Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, mchezo utakaofuata utapigwa nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kusafiri mkoani Shinyanga kuifuata Mwadui Fc
Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuikabili Dodoma Jiji na kwenda kumalizia ratiba yake ya duru ya kwanza mkoani Mbeya dhidi ya Ihefu Fc

ADVERTISE HERE