Mshambuliaji kiongozi wa Azam Fc, Prince Dube, ambaye aliumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga jana Novemba 25, anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kuvunjika mkono
Taarifa iliyotolewa na Azam Fc imebainisha kuwa Dube raia wa Zimbabwe, aliumia dakika ya 15 kwa kuvunjika mfupa wa mbele wa mkono wake wa kushoto unaoitwa Ulnar
Huu ni mfupa unaoanzia kwenye kiwiko na kushuka hadi kwenye kidole cha mwisho
Ataondoka nchini Jumapili ya Novemba 29 kkwa ndege ya Shirika la Kenya Airways (KQ)
Tunampa pole, tunamtakia kila la kheri kwenye matibabu yake
ADVERTISE HERE