Ndivyo ilivyokuwa jana kwa msemaji wa klabu ya Azam Fc Thabiti Zacharia maarufu Zakazakazi alipoishuhudia Azam Fc ikigeuka 'under-dog' mbele ya Yanga wakipigiwa mpira mwingi katika sebule yao, dimba la Azam Complex
Azam Fc walipoteana katika mchezo huo wakichapwa bao 1-0 na vijana wa Cedric Kaze katika mchezo ambao walishindwa kupiga hata shuti moja lililolenga lango
Kabla ya mchezo huo Zakazaki alitamba kuwa na uhakika wa kupata ushindi dhidi ya Yanga huku akiwaita mabingwa hao wa kihistoria kuwa ni under-dog mbele ya Azam
Lakini hakuamini alichokiona hapo Chamazi, jasho lilimtiririka mithiri ya mkulima anayepalilia shamba lake majira ya joto

ADVERTISE HERE