Ule mchezo wa kuamua nani anajipambanua kileleni mwa msimamo wa ligi kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga unapigwa uwanja wa Azam Complex saa moja usiku wa leo
Yanga ikiwa klabu pekee ambayo haijafungwa msimu huu, inakwenda Chamazi ikiwa na hesabu za kuondoka na ushindi ili kuendelea kutamba na rekodi hiyo
Lakini pia matokeo ya ushindi yatamaanisha kuwa mabingwa hao wa kihistoria watakwenda kukaa juu ya msimamo wa ligi
Hata hivyo hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ubora wa Azam Fc
Leo safu ya ulinzi ya Yanga ambayo iko chini ya manahodha Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto watapaswa kuwa makini sasa kuwachunga washambuliaji tegemeo wa Azam Fc Prince Dube na Obrey Chirwa
Dube amefunga mabao sita msimu huu wakati Chirwa ana mabao manne
Baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Namungo, Carlinhos leo atakuwa na jukumu jingine pale Chamazi kuhakikisha anakuwa chachu ya kupatikana ushindi
Carlinhos amehusika kwenye mabao manne ya Yanga ligi kuu msimu huu, akifunga mawili na kutoa pasi mbili za mabao
Akishirikiana na kina Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Michael Sarpong, wana jukumu la kuwapa furaha mashabiki wa Yanga leo
Timu hizi zimekuwa na ushindani unaokaribiana, hivyo ni mchezo ambao mashabiki watarajie kupata burudani