Azam Fc vs Yanga, mechi ya kibabe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Nov 2020
Azam Fc vs Yanga, mechi ya kibabe

Keshokutwa Jumatano, kikosi cha Yanga kitashuka dimba la Azam Complex Chamazi kuikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Huu ni mchezo muhimu kwa kila upande, mshindi wa mchezo huu atajihakikishia kusimama kileleni mwa msimamo wa ligi

Timu zote zimejikusanyia alama 25, Azam Fc iko kileleni kwa tofauti ya mabao tu

Miaka ya karibuni, Azam Fc imejijengea upinzani na Yanga kukiwa na ile dhana kuwa wao ni ndugu mmoja na Simba

Hilo huthibitishwa na ushindani wa mechi zinazozikutanisha timu hizo. Mara nyingi Azam Fc ikicheza na Yanga hucheza tofauti sana ukilinganisha na inapokutana na Simba

Takwimu zinaonyesha Azam Fc na Yanga zimekuwa na upinzani wa karibu sana

Kila moja imeshinda michezo nane, zimetoka sare michezo nane Yanga ikifunga jumla ya magoli 30 na Azam Fc ikifunga magoli 31

Msimu uliopita Azam Fc iliondoka na alama nne dhidi ya Yanga, ikishinda mchezo wa duru ya kwanza na ule wa duru ya pili ukimalizika kwa suluhu ya bila kufungana

Jumatano wanakutana katika mchezo ambao kila mmoja atakuwa na hesabu za kusaka ushindi

Kocha Cedric Kaze amekosa ushindi katika michezo mitatu iliyopita, huu sio mchezo ambao atakubali kuishuhudia timu yako ikipoteza na pengine hata kulazimishwa sare

Azam Fc wameamua kuupeleka mchezo huo katika uwanja wao, lakini mara nyingi Yanga imefanya vizuri kila ilipokutana na Azam Fc pale Chamazi

Mchezo wa mwisho timu hizo kucheza Chamazi, Azam Fc walichapwa mabao 2-1. Mabao ya Obrey Chirwa na Gadiel Michael

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’