Pamoja na Yanga kukosa ushindi muhimu dhidi ya Namungo Fc jana, tukio la mlinda lango Metacha Mnarta kudaka mkwaju wa penati kwenye dakika za majeruhi liliwapa furaha mashabiki ambao waliamua kumtuza fedha
Huu ni utamaduni kwa Yanga, mchezaji anapofanya jambo la kuwafurahisha Wananchi hutoka uwanjani na kibunda cha fedha


Namungo walipewa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 90 baada ya Bakari Nondo kumfanyia madhambi Shiza Kichuya ndani ya eneo la hatari
Mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
ADVERTISE HERE