Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo ambao walihitaji matokeo ya ushindi ili kushikilia usukani wa ligi
Ni kati ya ile michezo ambayo wachezaji wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo
Leo makosa yalikuwa mengi, nyota wa Yanga wengi hawakuwa mchezoni
Ni mchezo ambao Yanga imecheza chini ya kiwango, ilikuwa siku mbaya ofisini kwa wachezaji wengi
Farid Mussa, Tuisila Kisinda, Sarpong leo hawakuwa na siku nzuri wakati Mukoko nae akifanya makosa mengi eneo la kiungo
Yawezekana mapumziko ya wiki mbili yameathiri ile morali waliyokuwa nayo kabla ya ligi kusimama
Mchezo unaofuata wanaelekea kule Chamazi kuikabili Azam Fc ambayo ilipoteza mchezo jana kwa kufungwa na KMC bao 1-0
Bila shaka matokeo ya mchezo wa leo yatawaamsha kwani wakicheza hivi hawatapata matokeo dhidi ya Azam Fc
Sare tatu mfululizo sio matokeo mazuri kwa Yanga ambayo msimu huu imepania kupigania ubingwa wa 28