Mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc, umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1
Yanga ilitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 13 kupitia kwa Carlinhos aliyeunganishwa kwa kichwa krosi ya Kibwana Shomari
Hata hivi makosa ya Farid Mussa kupoteza mpira eneo la hatari yaliinufaisha Namungo kusawazisha kwenye dakika ya 17 kupitia kwa Stephen Sey



Katika dakika za majeruhi mlinda lango Metacha Mnata alifanya kazi ya ziada kuisaidia Yanga kuondoka na alama moja baada ya kuokoa mkwaju wa penati
Yanga leo imepoteza nafasi muhimu ya kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi, kwani wanaendelea kubaki nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 25 sawa na Azam Fc
Azam Fc wana uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa ukilinganisha na Yanga
Yanga imeendelea kuwa klabu pekee ambayo haijafungwa msimu huu
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Azam Fc Novemba 25