Azam Fc imepoteza mchezo wa pili msimu huu baada ya kuchapwa bao 1-0 na KMC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Uhuru
Matokeo hayo yanatoa nafasi kwa Yanga kupanda kileleni kwenye msimamo wa ligi kama watafanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Namungo Fc hapo kesho
Azam Fc wamebaki na alama zao 25 baada ya kushuka dimbani mara 11, wakati Yanga wana alama 24 wakizikusanya kutoka michezo 10
Simba imepata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya vibonde Coastal Union na hivyo kufikisha alama 23. Simba imeendelea kubaki kwenye nafasi ya tatu
Aidha Gwambina Fc nayo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliopigwa leo
Mchezo wa mapema ulizishuhudia Polisi Tanzania na Ihefu Fc zikigawana pointi baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana