Mapema leo uongozi wa klabu ya Yanga ulimtangaza Haji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi iliyoachwa na Patrick Simon ambaye amesimamishwa akichunguzwa na tuhuma za kuihujumu klabu
Mfikirwa ni mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, akiwa Mgurugenzi wa Fedha na Mipango
Huyu ni Mwanayanga kwelikweli, hakuna mwenye shaka na Uyanga wake

Muhimu kwake ni kuhakikisha anatimiza majukumu yake vyema ili kuongoza ndoto ya Wanayanga ambao wanahitaji kuona ubingwa ukirejea Jangwani kwa mara ya 28
Nafasi aliyopewa ni kubwa, katika kipindi cha miaka miwili yeye anakuwa mtu wa tano kushika nafasi hiyo
Mfikirwa amesema atahakikisha anasimamia na kufanikisha mipango yote ya klabu ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara
Mengine ni mabadiliko ya uendeshaji wa klabu na ujenzi wa hostel na Uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo Kigamboni. Amewaomba Wanayanga wampe ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake vyema