Mshauri Mkuu wa klabu ya Yanga Senzo Mazingisa amesema kuwa Rais wa GSM Ghalib Said Mohammed ni moja ya viongozi wa kipekee aliowahi kufanya nao kazi
Mazingisa ambaye alijiunga na Yanga miezi mitatu iliyopita, amemtaja GSM kama kiongozi asiye na makuu, wakati wote yupo kuwatumikia watu wake
"Ikiwa leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa, nachukua fursa hii kumtumia salam maalumu za kuzaliwa Rais wa GSM, Mr Ghalib Said"
"Ni kiongozi ambaye nadra sana kumpata, asiye mjivuni na asiyependa sifa wala kuonekana . Mara zote amekuwa mkimya lakini ni mpambanaji haswa akiwa anaongoza vikosi vyake kwa heshima na imani kubwa sana. Ni kiongozi asiyependa umaarufu, ni binadamu mwenye kujali maslahi ya watu wake"
"Heri ya kuzaliwa Rais wa GSM . Wewe ni miongoni mwa viongozi wazuri zaidi niliowahi kukutana na kufanya kazi pamoja. . Upo katika kiwango bora cha uongozi. . katika miezi michache uliyohusika katika kuijenga Yanga yetu tayari matokeo yake yameonekana ndani na nje ya Tanzania"