Wakati mwingine unaweza kuelewa kwa nini kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki wa Yanga wanaoamini kuwa wachezaji wao huwa hawapewi nafasi kwa makusudi tu wanapoitwa timu za Taifa
Alichofanya Fei Toto kwenye mchezo dhidi ya Tunisia jana ni somo kwa kocha Etienne Ndayiragije kuwa hapaswi kuingia kwenye siasa za hivi vilabu vikubwa kama anataka kufanikiwa katika timu ya Taifa
Mwenzie Emmanuel Amunike ambaye aliipeleka Stars michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika nchini Misri, aliukwepa mtego huu wa kulazimishwa kuwapa nafasi zaidi wachezaji wa timu moja
Inashangaza kuona Fei Toto hana nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Ndayiragije pamoja na kuwa kwa sasa ukizungumzia viungo bora wazawa, pengine yeye anaweza kuwa nafasi ya kwanza
Dakika 30 za mwanzo mchezo dhidi ya Tunisia hazikuwa nzuri, timu ilipoteana kati, viungo walikosa ubunifu
Lakini alipomuingiza Fei Toto kuchukua nafasi ya Himid Mao, mabadiliko yalionekana, timu ilianza kucheza mpira Fei akishirikiana vyema na Jonas Mkude na Farid Mussa ambaye alirudishwa kuongeza nguvu eneo la kiungo
Ni Fei Toto aliyefunga bao muhimu lililoipa Stars alama moja ambayo inaweza kuwasaidia katika kusaka tiketi ya tatu ya michuano ya Afcon
Ammunike hakuwa mnafiki, aliwahi kuzungumza waziwazi kuwa Fei Toto ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, anakosa vitu vichache sana ambavyo anaamini anaweza kuvirekebisha
Lakini alibainsiha kuwa Fei Toto ana uwezo wa kucheza klabu kama FC Barcelona ambayo yeye aliwahi kuitumikia
Ni bahati mbaya sana siasa hizi za Usimba na Uyanga zinapelekea wachezaji wenye vipaji kama kina Fei Toto wasipewe nafasi